{{menu_nowledge_desc}}.

CIFOR–ICRAF publishes over 750 publications every year on agroforestry, forests and climate change, landscape restoration, rights, forest policy and much more – in multiple languages.

CIFOR–ICRAF addresses local challenges and opportunities while providing solutions to global problems for forests, landscapes, people and the planet.

We deliver actionable evidence and solutions to transform how land is used and how food is produced: conserving and restoring ecosystems, responding to the global climate, malnutrition, biodiversity and desertification crises. In short, improving people’s lives.

Mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Msitu wa Londiani, 2018-2022

Export citation

Msitu wa Londiani ni miongoni mwa misitu mingi katika Kaunti ya Kericho. Msitu huu una eneo la hekta 9,015.50. Msitu ulitangazwa katika gazeti la serikali kupitia taarifa ya kisheria nambari 44 ya 1,932 kwa lengo ya kuuhifadhi. Ofisi ya msitu inapatikana katika kaunti ndogo (subcounty) ya Londiani katika Kaunti ya Kericho na inapakana na wilaya (division) za Chepseon na Kuresoi. Msitu umegawanywa katika viunga vitatu-Kedowa, Chebewa na Londiani-ambavyo pia vimegawanwa katika safu ya vitalu kwa urahisi wa usimamizi. Msitu wa Londiani unasimamiwa na meneja pamoja na watumishi husika wa KFS wakichangia katika usimamizi. Mhifadhi bonde ya Kaunti ya Kericho pia ana ofisi ndani ya msitu wa Londiani. Msitu uko karibu takriban mita 2,326 kutoka usawa wa bahari. Msitu huu ni kati ya misitu ya kwanza ambayo Mpango wa Uendeshaji Shirikishi wa Msitu (PFMP) uliendelezwa baada ya Sheria ya Misitu ya 2005 kupitishwa na kutekelezwa mwaka 2007. PFMP iliyotangulia ilizinduliwa mwaka 2012 na mkurugenzi wa Kenya Forest Service (KFS) na ilikuwa ya muda wa miaka mitano hadi Desemba 2016. Mwongozo wa PFM unahitaji kuwa miezi 6 kabla ya kukamilika kwa mpango huo, mchakato wa kupitiwa mpango unapaswa kuanza ili kuhakikisha kuwa mpango huo unafanyika kabla ya kikomo cha mhula. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa fedha, mchakato wa mapitio haukuanza hadi Oktoba 2017.
Download:
    Publication year

    2018

    Authors

    Kenya Forest Service

    Language

    Kiswahili

    Keywords

    forest management, community forestry, water resources

    Geographic

    Kenya

Related publications